SERIKALI
imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy la
kutaka taasisi za umma ziweze kununua mafuta ya kampuni hiyo yenye ubia
wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali ili faida inayopatikana itumike kwenye
kutatua changamoto za Watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa Mjini Dodoma mapema leo baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Puma Dk Ben Moshi kutoa ombi hilo kwa Waziri wa Fedha na
Mipango Dk Philip Mpango wakati wa tukio la kampuni hiyo kutoa gawio la
Sh bilioni 7 kwa Serikali ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na
biashara ya mafuta.
Akikubali
ombi hilo Dk.Mpango alisema kuwa watalifanyia kazi ombi hilo hasa kwa
kutambua hata mchango wa kampuni ambazo zimewekeza nchini na zina ubia
na Serikali, huku akitoa angalizo kuwa pamoja na ombi hilo
kufanyiwa
kazi,hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima ushindani uwepo ili
kupatikana kwa bidhaa bora."Serikali tumefurahi kwa gawio hili ambalo
mmelitoa kwani fedha hizi zitakwenda kuhudumia Watanzania masikiniambao
wanahitaji kupata huduma muhimu.Hivyo niwahakikishie Puma ombi lenu
nimelisikia na tunalifanyia kazi lazima tuendelee kushirikiana ili kuwa
na uwekezaji wenye tija kwa nchi yetu,"alisema Dk.Mpango.
Pia
alitumia nafasi hiyo kuitaka kampuni ya Puma kuendelea kufanya kazi yao
kwa ufanisi zaidi ili mwaka ujao wa fedha, gawio liongezeke zaidi na
kuwahakikisha Serikali inalo jicho lake ambalo linaangalia kwa kampuni
zote na mashirika ambayo wana ubia nayo.
Awali
kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh bilioni 7 kwa Waziri wa Fedha
na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi yaPuma Dk. Mosha alisema kuwa wanatambua
majukumu yao kwenye kufanyabiashara ya mafuta na ndio kampuniambayo
inaongoza kwenye soko lakini ombi lao kwa Serikali ni kwamba itoe
maelekezo kwa taasisi na mashirika yaumma kununua mafuta kutoka kwao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika,Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo pamoja na viongozi waanndamizi kutoka Wizara hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited Dkt.Ben Moshi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni ,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.

Dk Mapango akipongezana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti pamoja na Mwenyekiti wa Puma, Dkt. Moshi

Dk. Mpango akifafanua jambo kwa kusisitiza Taasisi mbalimbali za Serikali kuboresha huduma zao na kuipatia serikali gawio kubwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma, Philippe Corsalettti wakati wa hafla ya kampuni hiyo kukabidhi gawio la sh. bilioni 7 kwa serikali mjini Dodoma,pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...