Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

Kesi ya shambulio inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge mstaafu wa Mkuranga, Mhe. Adam Kighoma Malima na mwenzake kuanza kusikilizwa Agosti 9, mwaka huu.

Hatua hii imekuja baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelekezi na kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).

Katika hali hiyo, Malima anashtakiwa pamoja na Ramadhani Mohamed.Wamesomewa PH, na Wakili wa Serikali, Ester Martin mapema Leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage.

Katika maelezo hayo, Malima na Mohammed wamekubali maelezo yao binafsi, siku ya tukio kuwa walikuwepo Masaki, walikamatwa na kushtakiwa na wamekanusha tuhuma zote zinazowakabili.

Katika kesi hiyo, Malima anadaiwa kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali.Malima anadaiwa kumzuia afisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.
Kwa upande wa mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed Kigwande Naye anakabiliwa na shtaka la kumshambulia Mwita Joseph.
Ilidaiwa, Mei 15,2017 huko huko Masaki mshtakiwa Ramadhani akiwa na nia ya kumzuia Mwita Joseph ambaye ni afisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business Enterprises wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia na kumsababishia maumivu.
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana hadi Agosti 9, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...