Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa wanawaandaa watu kupiga picha katika eneo la Nje mara baada ya watu kujaa ndani na kulazimika kuongeza mashine ndani ya maonesho ya Sabasaba ambapo hitaji la watu kupata vitambulisho vya Taifa limekuwa kubwa
Msululu wa watu wakiwa katika eneo la nje ya banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakisubiri kupatiwa huduma kwa ajili ya kupata vitambulisho ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Hifadhi hati kutoka Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa 'NIDA' Bi. Rose Mdami akimsikiliza mmoja wa
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam aliyefika kupata huduma ya Kitambulisho
cha Taifa katika banda lao lililopo katika Viwanja vya Maonyesho
Sabasaba
Foleni ya kupata vitambulisho katika banda la ndani la NIDA ikiwa imeshika kasi kuliko kawaida hali iliyowalazimu kuongeza vifaa na watumishi wa kufanyakazi katika Viwanja vya Sabasaba
Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Bw. Said
Said akiwa amezungukwa na wananchi waliofika kupata
vitambulisho vya Taifa katika viwanja vya Maonesho Sabasaba katika eneo la nje na kuwapa maelzo namna ya kupata Vitambulisho vya Taifa
Sehemu ya wananchi wakiwa wamekaa chini wakisubiri foleni yao ifike ili waweze kuchukua Vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA
Maofisa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) wakiwa Wamezungukwa na wananchi waliofika kupata
vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba.
Picha na Humphrey Shayo, Gobu ya Jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...