BENKI ya NMB imedhamini mashindano ya mchezo wa Golf yaliyoandaliwa
na Club ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa club hiyo.
Michuano
hiyo mikali na ya kipekee iliyopambanisha wachezaji wa mchezo wa golf
kutoka club mbalimbali ilifanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam na
washindi mbalimbali wa mchezo huo kujishindia tuzo baada ya kuibuka
kidedea hatua mbalimbali.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ndiye mgeni rasmi aliyewaongoza wageni
mbalimbali waalikwa kwenye hafla ya kuwakabidhi tuzo washindi kabla ya
kuyapongeza makampuni mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB iliyofanikisha
michuano hiyo.
Menaja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko akimkabidhi tuzo ya
ushindi wa mchezo wa Golf, Bi. Tayana William katika michuano ya mchezo
huo maalumu kwaajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Clabu
ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilidhamini mashindano
hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kushirikisha wanamichezo
mbalimbali.
Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi
wa mchezo wa golf, NMB ilipata fursa ya kukabidhi tuzo sita kwa washindi
mbalimbali, wakiwemo; Samwel Mosha, Chiku Eliasy, Tayana William, Eric
Tango, Vicky Elias pamoja na Mohamed Rahim aliyetwaa tuzo ya mshindi wa
Jumla wa mchezo huo. Hata hivyo, katika hafla hiyo Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe pia aliikabidhi
Benki ya NMB na makampuni mbalimbali tuzo ya shukrani iliyotolewa na
Uongozi wa Club ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam kutambua mchango wa
benki hiyo na taasisi zingine katika mafanikio ya mchezo wa Golf.
Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko akimkabidhi tuzo ya
ushindi wa mchezo wa Golf, Samwel Mosha katika michuano ya mchezo huo
maalumu kwaajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Clabu ya
Gymkhana ya jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilidhamini mashindano
hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kushirikisha wanamichezo
mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...