Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akifungua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi huo mkubwa wa maji kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Antony Sanga wakati alipoanza ukaguzi wa mradi huo kabla ya kuufungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Eng. Gerson Lwenge wakati akielekea kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Kada maarufu wa CHADEMA kanda ya Ziwa Hamis Tabasamu mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na waandishi wa habari mbalimbali wa mkoani Mwanza ambao walishiriki katika kazi ya ufunguzi wa mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...