--
Diwani
Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya
Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni
kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa Sh.5,000,000/=.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa
walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa
mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho
cha pesa alitakiwa na watuhumiwa kuwapa rushwa ya Sh.10,000,000/=
Inadawaiwa Watuhumiwa
walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati
ya mipango miji inashughulikia maombi ya
kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha
ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.
Uchunguzi
wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na
kifungu namba 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka
2007 wamepewa dhamana.
Mkuu
wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bi.T. MNJAGIRA anawaasa Viongozi wote wa Umma,
Wanasiasa na Watumishi wote wa Serikali, kuheshimu nyadhifa zao na kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Pia,
anatoa wito kwa Wananchi wote kuendelea
kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa ili waweze kuchukuliwa
hatua za kisheria, Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumezuia vitendo hivyo
visiendelee kujitokeza katika Jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...