Lengo ni kuwafikia waliowengi na huduma za kibenki kwawasio na akaunti za benki.
Dar es Salaam Tanzania, Jumatatu 14 Agosti 2017 – Ikiwa ni moja kati ya mikakati yake ya kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa huduma kwa kila mtanzamia hasa kwa wale wasio na akaunti za Benki, Benki ABC Tanzania leo imezindua huduma za wakala itakayowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki hiyo wakiwa katika mazingira yeyote yale.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi Bi.Joyce Malai alisema Benki ABC inaendelea kuja na teknolojia mpya katika utoaji huduma ili kukidhi mahitaji ya kibenki kwa wateja wake nchini Tanzania.
Changamoto ya Kipato kidogo na kuhitajika kwa vielelezo vingi wakati wa kufungua akaunti za Benki pamoja na uhaba wa huduma za kibenki kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini yamefanya Watanzania wakose huduma za kibenki na hivyo kufanya maendeleo ya kiuchumu ya nchi kuwa finyu. Sisi Benki ABC tumejiandaa kuhakikisha kwamba huduma za uwakala za Benki yetu zinakuwa ni suluhisho kwa Watanzania kupata huduma bora za kifedha wakiwa popote bila ya kupata shida, alisema Joyce.
Aliongeza kuwa kama Benki inayokua kwa kasi hapa nchini, benki ABC inalengo kupanua huduma na uwepo wake kwenye miji mikubwa hivyo huduma za uwakala zitakuwa ni moja ya njia ya kufikia malengo hayo.
Joyce aliongeza kuwa huduma za uwakala za Benki ABC itakuwa na tija kwa Watanzania ambao hawana akaunti za Benki na pia kwa wale ambao wana akaunti lakini badala ya kupoteza muda mwingi kupanga foleni kwenye matawi yao wanaweza kupata huduma hizo kwenye wakala wa Benki hiyo popote pale. Huduma za wakala zitaanza kupatikana jijini Dar es Salaam kupitia Maxcom Afrika. Wateja wa Benki ABC watapata huduma zote za kibenki kupitia wakala wote wa Maxmalipo kwa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya huduma hiyo kusambaa nchini kote.
Meneja wa Kitengo Binafsi Benki ya ABC
Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari wa uzinduzi wa huduma za uwakala wa
Benki hiyo kwa kushirikiana na Maxcom Africa Plc.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa Plc Jameson Kasati akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari jana kwenye hafla ya kushirikiana na Maxcom Africa Plc kutoa huduma za kibenki.
Meneja huduma za uwakala wa Benki ABC Mwita Robi akionyesha mashine ya uwakala wa huduma za kibenki jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindua huduma za hiyo jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa Plc Jameson Kasati akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari jana kwenye hafla ya kushirikiana na Maxcom Africa Plc kutoa huduma za kibenki.
Meneja huduma za uwakala wa Benki ABC Mwita Robi akionyesha mashine ya uwakala wa huduma za kibenki jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindua huduma za hiyo jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...