Katika kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.

Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali inayochochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo. 
Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo. 
Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe (wapili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege. 
Maafisa kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa.  
Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...