Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro amezindua mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia ‘GBV Prevention Project’ unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Agosti 14,2017 katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto wakiwemo wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,maafisa watendaji wa kata,maafisa tarafa,afisa maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii,afisa utamaduni na dawati la jinsia na watoto.
Akizungumza wakati wa kuzindua mradio huo,Matiro alilipongeza shirika hilo kwa kuelekeza nguvu zake katika mapambano dhidhi ya ukatili wa kijinsia ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii husika kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wahusika wanapobainika.
“Serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali,ili mfanikiwe mnatakiwa mshirikishe wadau kwenye maeneo husika,mmefanya jambo jema kujitambulisha badala ya kuanza kutekeleza mradi kimya kimya kama baadhi ya mashirika vile yamekuwa yakifanya hali inayowafanya washinde kufanikiwa”,alieleza Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud,kushoto ni Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...