Na Fredy Mgunda,Iringa
Halmashauri ya wilaya ya
kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji
mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827
kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto
hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara
ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye
ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa
wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa
Ilula.
“Leo nimefika hadi huku
kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda
mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani
ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua
matatizo ya wananchi”alisema Masenza
Aidha Masenza alisema kuwa
wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania
dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi
wake.
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa
uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka
kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha
wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.

Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula

Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...