Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amesema kuwa Serikali haina mpango wa kutoa vibali kwa ajili ya kuuza shehena ya kinywaji aina ya viroba vilivyopo stoo kwenye maghala ya Wafanyabiashara wa pombe hiyo.

Aliongea hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika ghala la kampuni ya usambazaji wa vinywaji aina ya kiroba ya Temani iliyopo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa Serikali ilitoa muda mrefu kuanzia mei 2016 mpaka machi 2017 kwa wenye shehena hiyo ya viroba kuuza na kumaliza mzigo wote uliopo stoo hivyo basi baada ya Serikali kupiga marufuku pombe hiyo, hakuna kibali kitakachotolewa kwa ajili ya kuuza shehena ya mzigo wa viroba uliobaki. 

Akiongea kwa Mh. Waziri , Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bi Elizabeth Massawe alisema wanaiomba Serikali iwasaidie ili waweze kupunguza mzigo mkubwa wa viroba ambao wanao katika ghala lao sababu wanapata hasara kubwa na wanatakiwa kulipia kodi ya magahala waliyokodi. .

Katika ziara hiyo ya kutembelea ghala la vinywaji la kampuni ya Tema Enterprise Waziri alikuta shehena kubwa ya katoni 150,000 za viroba zilizofungashiwa katika vifuko vya plastiki.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Temani ambayo wana ghala la kuhifadhia vinywaji aina ya viroba lililoko Kimara Temboni Bibi Elizabeth Massawe (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ghala hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani lililopo Kimara Temboni.


Sehemu ya vinywaji aina ya viroba na vifungashio vilivyopo katika ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...