Jeshi la Ulinzi la Wananch wa Tanzania linapenda
kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya majeshi yanayoanza tarehe 25 Agosti 2017. Sherehe hizi ni za kuadhimisha siku ya kuanzishwa
kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo hufanyika kila mwaka
tarehe 01Septemba, mwaka huu sherehe hizo zitaadhimishwa wakati Jeshi
linatimiza miaka 53 tangu lilipo
asisiwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza Marehemu Baba wa Taifa Mwl Julius
Kambarage Nyerere Septemba Mosi 1964.
Mwaka huu 2017 maadhimisho hayo yatafanyika kwa
wanajeshi kufanya shughuli mbalimbali kuanzia tarehe 25 Agosti 2017 hadi tarehe 31
Agosti 2017 na kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 01 Septemba 2017.Shughuli hizo ni
pamoja na kufanya shughuli za huduma za kijamii katika maeneo jirani na vikosi
vya Jeshi, Wanajeshi kuchangia damu salama katika hospitali mbalimbali nchini,
kutoa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa Dar es salaam huduma za tiba
zitatolewa katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi siku ya
tarehe 01 Septemba, aidha wanajeshi watafanya michezo mbalimbali na wananchi Pamoja
na kushiriki kufanya usafi kwenye maeneo ya kijamii (Hospitali, Masoko, Mashule
n.k) na pia watafanya michezo Shirikishi na jamii inayowazunguka.
Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ni Wiki ya Majeshi na Afya yako.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari
na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...