
Akizungumza
zaidi mmoja wa Madereva wa dala dala katika mgomo huo (hakutaka
kujitambulisha jina),alisema kuwa wao hawawezi kulipa tozo hiyo wakati
miundombinu ya kituo hicho si rafiki na hairidhishi kabisa kwa vyombo
vyao vya usafiri.
"ni
vyema wakazirekebisha kwanza changamoto kadhaa zilizopo hapa
kituoni,kisha baadae waje na huo mkakati wao wa kutupandishia hiyo tozo
yao,lakini kwa sasa itakuwa vigumu kulipa kwa sababu kama unavyoona
mazingira yalivyo hapa kituoni",alisema mmoja wa Madereva.
Mpiga
picha wa Globu ya Jamii pamoja na kuonja joto ya jiwe ya kukosa
usafiri,pia alijionea adha waliokuwa wakiipata abiria wengine
waliokuwepo kituoni hapo,huku baadhi ya abiria wakilazimika kutumia
usafiri wa piki piki kuwahi kwenye shughuli zao na wengine wakitembea
kwa Miguu.
Mpaka Globu ya Jamii inaondoka kituoni hapo ufumbuzi bado ulikuwa haujapatikana.
Madereva na Makondakta wakijadiliana kufuatia mgomo huo
Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri kituoni hapo mapema leo asubuhi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...