
MWEKA
HAZINA wa miaka mingi wa Kilimanjaro Band, ambaye alijulikana kwa
wapenzi wengi kutokana na kuwa mkata tiketi wa bendi wa miaka mingi
sana, Francis Mnguto, maarufu kwa jina la Babu Francis amefariki leo
alfajiri nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam.
Kwa
miezi kadhaa Babu Francis amekuwa akisumbuliwa na tatizo la figo.
Taarifa kutoka kwa familia ni kuwa mazishi yatakuwa Dar es Salaam
Jumatano 23 Agosti. Msiba upo nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...