Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
Na.
Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.
Serikali kupitia Idara
ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa
kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.
Akizungumza katika
makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya
Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi
lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho
kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa
taaluma rasmi kama zingine.
“Leseni hizo zimeanza
kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada
ya hapo wale amabo watachapisha magazeti
na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la
jinai”, alisema Dkt. Abasi.
Katika zoezi hilo Dkt.
Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa
na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo
ambayo ni magazeti ya Serikali.
Dkt. Abbasi ametoa wito
kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado havijaanza taratibu za upataji wa
leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano
na usumbufu usio wa lazima.
“Nitumie fursa hii
kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN)
walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo,
hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi
wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake Mhariri
Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza
agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa
kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.
“Ukifanya kazi kihalali
unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya
biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...