WADAU
wa maji na Mazingira washauriwa kushirikiana ili kukidhi mahitaji ya
maji kwa wakazi wa Dar es Salaam pia washauriwa kutoa namba maalumu ya
simu kwaajili ya wananchi waonapo tatizo la maji au maji kutiririka
katika maeneo mbalimbali ili kuondoa upotevu wa maji katika mkoa wa Dar
es Salaam.
Hayo
ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati akizungumza na
wadau wa maji pamoja na wadau wa Mazingira jijini Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa Wadau wamaji wanatakiwa kushirikiana na ili kupunguza
upotevu wa maji kutokana na ubovu wa miundo mbinu ya maji.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, usambazaji wa maji
Haruni Josef Kwa upande wake DAWASCO wamewaomba wadau wa maji ili kuendeleza na kukuza maendeleo ya kwaajili ya kujenga mtandao wa maji kwaajili ya kuyasafirisha ili yamfikie kila mwananchi wa jiji la Dar es Salaam.
Wadau
waliokutana leo ni Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), wizara
ya Afya, DAWASCO,DAWASA, WATERAID na wadau wa mazingira kwa pamoja
wakiwa na kauli mbiu ya maji ni uhai na usafi ni utu.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wadau wa maji safi
pamoja na wadau wa maji taka ili kutatua changamoto za maji katika jiji
la Dar es Salaam.Pia ameshuhudia kusaini makubaliano kati Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam na Taasisi ya Borda ya hapa nchini.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akishuhudia taasisi ya Borda na Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya wadau ya maji wa maji
safi na wazingira walipokutana leo leo kufanya mazungumzo ya wadau wa
maji pamoja na wadau wa mazingira.
Wawakilishi
wa Kampuni ya Jamka Enterprise Company wakipokea hundi ya shilingi
milioni Tano ambazo wamekopeshwa na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania (UTT) leo mara baada ya kikao cha Wadau wa Maji na Mazingira
kufunguliwa jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kuzungumza masuala ya
maji na mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...