Jonas Kamaleki- MAELEZO.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ameridhia mwekazi
kupewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kijijini Msoga, Wilayani Chalinze,
Mkoa wa Pwani.
Waziri
Lukuvi amesema kuwa wanakijiji wana uwezo wa kutoa ardhi hadi ekari hamsini tu zaidi
ya hapo ni Mhe. Rais mwenye uwezo wa kutoa hati kwa mwekazaji, hivyo alikwenda
Msoga kujiridhisha kabla ya kumshauri
Rais kutoa hati kwa mwekezaji.
Aliwauliza
wananchi katika mkutano uliofanyika kijijini Msoga kama walikubaliana kumruhusu
mwekazaji wa Region Recycling East Africa Limited kujenga kiwanda kijijini
hapo, nao wananchi kwa pamoja walisema kuwa ndiyo walitoa ardhi yao kwa ajili
ya uwekezezaji huo.
Kiwanda
hicho kitakuwa kinatumia betri mbovu za gari na za umeme jua (Recycling)
kama malighafi ya kutengeneza betri nyingine kwa ajili ya matumizi ya magari na
mitambo ya umeme jua. Mwekezaji huyo alipewa jumla ya ekari 56 na wanakijiji wa
Msoga kwa ajili ya uwekezaji huo.
“Vijiji
vilivyopimwa kimji vitaiingizia Serikali mapato na wananchi pia watapata fursa
za kupata mikopo kwenye mabenki na kufanya biashara kubwa,”alisema Lukuvi na
kuongeza kuwa anazishauri Halmashauri zote nchini kupandisha hadhi vijiji vya
namna hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...