Baada ya Soko la Sido kuteketea kwa moto,hatimaye Serikali Mkoani Mbeya imeridhia Waathirika wa janga la Moto katika soko hilo kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagizwa kujenga  vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.

Akitoa maelekezo ya serikali,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi na hatimae kuendelea na biashara zaoa kama kawaida.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbeya Mjini,Mkoa ikiwa ni pamoja na mbunge wa Jimbo  Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamoja na Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wathirika hao.Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ,Mkutano huo ukaridhiwa kuwa fedha hiyo ibaki kwa Mkuu wa Mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makala ameliagiza Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vifaa vya kuzuia moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.

 Naibu Spika ,Mhe.Dkt Tulia Ackson akimuonesha jambo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Amos Makalla mara baada ya kufanya mkutano na Wanyabiashara wa Soko la Sido-Mwanjelwa jijini Mbeya mapema leo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na jeshi la polisi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla wakitembelea eneo la soko la Sido lililoteketea Kwa Moto hivi karibuni Jijini Mbeya.


Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido-Mwanjelwa,wakifurahia uamuzi uliotoewa na Serikali ya Mkoa wa Mbeya,kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine.

Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amos Makalla alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa pamoja katika kutoa maamuzi ya kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine huku utaratibu wa ujenzi ukiendelea kuwekwa sawa.

PICHA ZOTE NA FADHIL ATICK MR.PENGO MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...