Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imejipanga katika masuala ya michezo kutoa nguvu pamoja na kuenzi michezo ya shule za misingi na Sekondari ili kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya Kikanda na Dunia na wachezaji kurudi medali za dhahabu.
SERIKALI imejipanga katika masuala ya michezo kutoa nguvu pamoja na kuenzi michezo ya shule za misingi na Sekondari ili kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya Kikanda na Dunia na wachezaji kurudi medali za dhahabu.
Hayo ameyasema leo Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akipokea bendera ya Taifa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo ambao walishiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) hivi karibuni, amesema wanafunzi wameonesha vipaji na kuweza kushika na nafasi ya tatu katika mashindano hayo.
Amesema kuwa shule zilizoshiriki zimeweza kutangaza Tanzania hivyo katika mashindano yajayo nguvu itaongezeka kwa sekondari nyingi kushiriki na kasha kuweza kupata wachezaji mbalimbali ikiwemo timu ya taifa pamoja na riadha.
Dk. Mwakyembe amesema kuwa katika Wizara hiyo atahakikisha wanafnaya vizuri katika michezo kwa kuweza kupata ushindi ikiwa kwa vilabu vyote vya michezo kujipanga.
Amesema katika michezo hakuna uchawi kinachohitajika ni juhudi na maarifa kwa wachezaji wanavyoshiriki mashindano yeyote ya ndani na ya nje ya nchi.
Aidha amesema wanafunzi walioshiriki na kushika nafasi ya tatu waongeze juhudi katika mashindano yajayo waweze kuwa washindi wa kwanza katika mashindano ya (FEASSSA).

Waziri
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza
baada ya kupokea Bendera kwa wanafunzi wa Shule ya Makongo walioshiriki
mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki
yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...