Ni msimu mwingine wa Soko la Wazi la Mkulima
Market maarufu kama Mkulima Soko. Tunakukaribisha kuungana na wazalishaji na
wachakataji bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi na uwindaji kuona wazalishaji
kutoka kila pembe ya Tanzania.
Katika Mkulima Soko utapata fursa ya kuona,
kupata elimu na kununua bidhaa bora zinazozalishwa Tanzania.
Soko hili la Wazi litafanyika kuanzia tarehe
30 Agosti hadi 2 Septemba 2017 (Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi). Karibu
ujifunze ufugaji wa sungura, samaki na nyuki. Kama kawaida soko litafanyika
kwenye Maegesho ya Magari ya Research Flats, mbele ya Jengo la Ndaki ya Kilimo
na Teknolojia za Uvuvi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Msimu huu kutakuwa na
wazalishaji wapatao 60 watakaoleta bidhaa mbalimbali fresh na zilizochalatwa.
Katika soko hili kutakuwa na mambo makubwa
manne na ili kuyajua mambo hayo manne .... BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...