WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara wa kumbukumbu.

Mnara huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa Afrika, ambapo zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia zao na nchi wanazotoka.

Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo hilo jana (Ijumaa, Agosti 25, 2017) na kuweka shada la maua katika mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na kuoneshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.

Akiwa katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu iliyotengwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki), Bw. Jose’ Prieto Cintado alisema mnara huo umejengwa kwa lengo la kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.

Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya Cuba inathamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa hao katika vita ya ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo iliamua kujenga mnara wa kumbukumbu katika nchi yao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .August 25/2017 wakiangalia Sanamu ya aliyekuwa Raisi wa Msumbiji Hayati Samora Masheli ambayo ipo katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliopo Havana Cuba Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .kulia pamoja na Mama Mary Majaliwa ,kushoto pamoja na mwenyeji wao katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .wakiweka Shada la Maua August 25/2017 katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliyopo Havana Cuba .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...