Na Edda Sanga, Mkurugenzi Mtendaji TAMWA
Wanaharakati wenzangu, karibuni TAMWA, mahali adhimu ambapo tumeamua kuzindulia maadhimisho ya miaka 30 ya Chama Cha Wandishi Wa Habari Wanawake Tanzania.
Jina la TAMWA si geni masikioni mwa Watanzania walio wengi, ikizingatiwa hiki ni chama kikongwe cha wanahabari Tanzania ambacho mithili ya chombo baharini, kimehimili mawimbi, makubwa na madogo, mitikisiko na misukosuko ya hapa na pale, na bado kikaweza kuelea katika bahari tulivu. Itoshe kusema, tumetoka mbali.
Mimi mbele yenu ni mmoja wa waasisi wa Chama Cha TAMWA, kwa niaba ya wenzangu kumi na mmoja, tulio hai ni kumi, ambapo wawili wametangulia mbele za haki. Namshukuru Mungu ametujalia neema ya kuuona Mwaka uliotutunuku fursa ya kuanzisha Chama hiki, japokuwa tunazindua harakati za maadhimisho haya, tukiwa na takriban siku 78 kufikia kilele hapo tarehe 17 Novemba Mwaka huu.
Tungependa ndugu zetu, marafiki zetu, wadau wetu, Watanzania wenzetu mmoja mmoja na katika ujumla wenu, muungane nasi kufurahia fursa hii ya kuadhimisha siku hii muhimu ambayo katika historia ya kuwepo kwetu, tunahesabu mafanikio lukuki tuliyoyapata.
Moja ya mafanikio hayo ambayo ni vigumu kusahau ni ushawishi, kuzengea na kuzonga kuliko fanyika kwa ustadi mkubwa , tukiwa na wenzetu TGNP, TAWLA, MEWATA, WLAC, LHRC, CRC na mashirika mengine kama hamsini hivi tukitetea kubadilika kwa sera, na sheria kandamizi zinazomnyima haki mwanamke na mtoto, hasa mtoto wa kike. Furaha yetu ilikamilika , pale Mwaka 1998 tulipofanikiwa kuongea na wabunge, wakatuelewa na kuwazawadia Watanzania SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA , maarufu kama SOSPA. Utakumbuka pia sheria hii iliboreshwa Mwaka 2005.
Uzuri wa sheria hii ya SOSPA, ni kwamba kwa mara ya kwanza, ilitamkwa wazi kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, ikampa mtoto wa kike ulinzi wa kutofanyiwa ukatili akiwa chini ya umri wa miaka 18.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Edda Sanga, akisoma tamko la uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho jijini Dar es salaam leo. Wengine ni wanachama wanzilishi wa TAMWA

 Bi Fatma Aloo akielezea jambo wakati wa mkutano huo
Mkutano wa uongozi wa TAMWA na wanahabari ukiendelea jijini Dar es salaam leo. Kusoma tamko kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...