Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma (mwenye koti
jeusi) akielezea jambo wakati wa ziara ya kamati hiyo
ilipokutana na mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri-TMA na
menejiment ya TMA (hawapo pichani), kwenyea ukumbi wa
mikutano wa TMA, Ubungo Plaza.
NA MONICA MUTONI
Siku ya Ijumaa, tarehe 25/08/2017, Kamati ya Ardhi na
Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ilitembelea
Makao Makuu ya Ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) yaliyopo jengo la Ubungo Plaza Dar es salaam ili kuona na
kupata taarifa mbali mbali za taasisi hiyo.
Taarifa ya utendaji ya TMA iliwasilishwa na ndugu Selemani
Selemani (Mchumi) pamoja na mambo mengine aliwafahamisha
wajumbe wa kamati hiyo kuwa Mamlaka imepokea ‘Certificate of
Appreciation’ toka Idara ya kukabililiana kamisheni ya kukaliana na
maafa na Mamlaka ya usafiri wa majini (ZMA) kwa kazi nzuri
inayofanywa ya kutoa huduma za hali ya hewa katika visiwa vya
Unguja na Pemba.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe, Mwenyekiti wa kamati hiyo
ya Ardhi na Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.
Hamza Hassan Juma alisifu kazi nzuri inayofanywa na mamlaka
katika kutoa huduma za hali ya hewa Zanzibar. Aliielezea
menejiment ya TMA kuwa, huduma za hali ya hewa nchini zinazidi
kuimarika hususan kwenye usahihi wa taarifa zinazotolewa kama
vile utabiri wa kila siku na tahadhari, hivyo kuongeza imani kwa
wananchi katika ufuatiliaji wa taarifa za hali ya hewa ukilinganisha
na hapo awali ambapo jamii ilikuwa na hulka ya kupuuzia taarifa
hizo.
Mhe. Juma alifahamisha mchango wa TMA unatambuliwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) akitolea mfano wa
pongezi zilizotolewa kwa Mamlaka na Makamu wa Pili wa Rais
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
Kwa upande mwengine, Mwenyekii wa Bodi ya Ushauri ya TMA
Dkt. Buruhani Nyenzi aliwashukuru wajumbe hao kwa pongezi
zilizotolewa na kuahidi kuisaidia Mamlaka kufikia malengo ya juu
zaidi katika utoaji huduma kwa kuboresha miundo mbinu. Aidha
aliwaeleza wajumbe hivi karibuni alikuwa na ziara ya kutembelea
vituo vya hali ya hewa vya unguja na pemba ili kujionea hali halisi,
hivyo wananchi wategemee huduma bora zaidi kwa kuwa lengo la
Mamlaka ni kuongeza na kuviboresha vituo vyake na kuongeza
usahihi wa takwimu za hali ya hewa zinazokusanywa.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru
wajumbe na kueleza utendaji kazi wa Mamlaka kwa kuzingatia
weledi na ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wenyewe na
wadau wa hali ya hewa, Aidha, Dkt. Kijazi alijivunia uwepo wa
wataalam wa sayansi ya hali ya hewa wenye sifa za kitaifa na
kimataifa ambao mchango wao mkubwa umeonekana katika
kuongeza usahihi wa taarifa zitolewazo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...