Asteria
Muhozya na Zuena Msuya, DSM
Serikali
imesema kuwa ifikapo tarehe 30 Agosti, mwaka huu itatangaza Zabuni ya kuanza
ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 2,100 katika Maporomoko
ya Maji ya Mto Rufiji. (Stiegler’s Gorge).
Hayo
yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kalemani
alitoa wito kwa Watanzania, Taasisi Binafsi na Kampuni zenye uwezo kutoka ndani
na nje ya nchi kujitokeza kuomba zabuni hiyo mara baada ya kutangazwa na
kuongeza kuwa, Serikali inazo fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi husika.
Aliongeza
kuwa, tayari taratibu za awali za utekelezaji wa mradi huo zimekwisha anza
ambapo Wataalam kutoka ndani na nje ya nchi wamekwishakutana na kupitia nyaraka
za mradi ikiwemo kuchagua eneo ambalo mradi husika utajengwa.
Watalaam
mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) wakielendelea na kazi ya kukamilisha nyaraka mbalimbali kuhusu mradi
husika.
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kutangazwa Zabuni ya Mradi wa Kuzalisha umeme wa Rufiji. Wanaofuatilia
ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...