Na
Mathias Canal, Singida
Vijana wametakiwa
kusimamia misingi ya Nidhamu ndani na nje ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi kwa kuhuisha mshikamano ili kulinda misingi ya Utaifa na
uwajibikaji kwani wao ndio nguvukazi ya Taifa na ushindi wa Chama Cha Mapinduzi.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi kwenye mkutano
wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa shule ya Sekondari
Ikungi.
Mhe Mtaturu alisema kuwa Dhana ya
Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama
na Jumuiya zake hivyo kuimarisha nidhamu, mshikamano na upendo ndio
silaha pekee itakayoleta heshima ndani ya jumuiya ya vijana wa CCM ili iweze
kusonga mbele zaidi na kuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha kipato cha
vijana.
Alisema kuwa Nia ya UVCCM ni kujenga
na kudumisha haiba njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya
kweli, yenye kuchunga adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila
mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...