Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na waandishi wa habari uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupeleka wanafunzi 75 kwenda kusoma vyuo vikuu vya nchini India jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Afisa Global Education Link (GEL) akipitia nyaraka mbalimbali za wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nchini India katika uwanja wa ndege wa mwalim Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Global Education Link (GEL) imesema kuwa sekta ya viwanda inahitaji rasilimali yenye ujuzi wa kuweza kuendesha sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa katika kasi ya serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Linki(GEL), Abdulmalik Mollel wakati akipeleka wananfunzi 75 wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya India, amesema vijana wanaokwenda kusoma ndio rasilimali ambayo itatumika katika sekta ya viwanda kutokana na ujuzi na maarifa watayotokanayo huko.
Amesema kuwa vijana wanakwenda kusoama katika nchi ambazo ziko mbele katika masuala ya viwanda hivyo
wataweza kutumika kuwa rasilimali ya viwanda nchini.
Mollel amesema katika kipindi kifupi katika mwaka huu zaidi vijana wamekwenda kusoma katka vyuo vikuu katika nchi za China pamoja na India.Amesema kuwa vijana wanaokwenda china wapo walikwenda kusomea wamepeleka wanafunzi 75 kati yao 50 ni sekta ya afya katika kozi za medicine, radiology, pharmacy na wengine waliobaki ni katika fani ambazo zinajihusisha na ukuaji wa viwanda ambazi ni Ufundi Makenika, Uhandisi wa Kemikali, Uhandis wa Umeme,Sayansi ya Chakula na Teknolojia, Uhandisi wa Tehama,pamoja na Uhandisi wa Petroli.
Aidha amesema kuwa Global inaendelea kupokea wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje milango iko wazi katika viwanja vya saba saba na Dar es Salaam, Mwanza Arusha, Dodoma pamoja na Zanzibar na nchi jirani Zambia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...