Na Bearice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo amesema kuwa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika (ALHP) una historia adhimu kati ya Tanzania na Afrika Kusini na itasaidia kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Mhe. Jaffo ameyasema hayo leo Wilayani Kongwa, Dodoma wakati wa ziara ya Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Watalamu wa Programu hiyo kutoka Tanzania na Afrika Kusini  kujionea maeneo yaliyotumika wakati wa  Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo Afrika Kusini. 
“Nchi ya Tanzania na Afrika Kusini zina urafiki mkubwa na wa karibu kuliko nchi nyingine yeyote Afrika, hivyo kupitia Programu hii tutazidi kuimarisha udugu na uhusiano uliopo” amefafanua Mhe. Jaffo.
Ziara hiyo ilihusisha maeneo ya makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini, Kambi walipokuwa wanaishi, mahandaki walipokuwa wanajihifadhi dhidi ya maadui pamoja na madarasa yaliyotumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru. 
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo akiongea na wajumbe wa Mkutano wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kutoka Tanzania na Afrika Kusini walipokuwa ziarani Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Serikalini Bi. Plumla Williams akitoa neno kwa niaba ya wajumbe kutoka Afrika Kusini walipotembelea maeneo ya ukombozi yaliyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya agenda ya Mkutano kuhusu utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurungenzi Mkuu wa Kazi za Umma kutoka Afrika Kusini Bw. Mziwonke Dlabantu (kulia). Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi.
Baadhi ya Viongozi kutoka Afrika Kusini wakiangalia makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini yaliopo Wilayani Kongwa, Dodoma. Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...