Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan Makeke.
Msanii wa mitindo inayohusu utamaduni wa Mwafrika Jocktan Makeke / MAKEKE INTERNATIONAL anatarajia kwenda Abuja Nigeria kwa ajili ya maonesho makubwa ya utamaduni ya FACE OF CULTURE NIGERIA, ambapo ataonesha mavazi yenye ubunifu wa hali ya juu ambayo yanakwenda kwa jina la #OTOSIM2017
Tamasha hilo litafanyika siku ya tarehe 09/09/2017 katika ukumbi wa Sheraton Hotel ya mjini Abuja.Aidha maonesho hayo yataambatana na utoaji wa tuzo kwa watu mbalimbali ambao wamefanya vizuri kwenye mambo ya utamaduni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...