Katika
kuboresha huduma za kibenki nchini Maendeleo Bank lao imetoa zawadi
kwa washinidi wake wanne wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya
‘Maendeleo pamoja na wewe’ iliyochezeshwa tarehe 31/8/2017 Jijini Dar es
salaamHafla ya kuwapatia washindi hao zawadi ilifanyika leo katika
ukumbbi wa ‘Mviringo hall’ uliopo makao makuu ya Benki hiyo ‘Luther
House’ posta Jijini hapa ambapo washindi hao wanne walijishindia zawadi
tofauti tofauti ikiwemo Ada za shule, tani za Saluji,Mabati pamoja na
kiwanja,
Akizungumza
katika hafla hiyo fupi mkuu wa kitengo cha biashara Maendeleo Bank
Peter Tarimo amesema katika kuhakikisha Maendeleo Bank inakuwa karibu
na wateja wao imeamua kuwahamasisha hasa wazazi kufungua Account za
Benki kwa ajili ya watoto wao ili kuweza kuwajengea utamaduni wa
kuhifadhi fedha
“Mtakumbuka
kuwa kampeni hii ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa nane na wateja
wengi walishiriki, Droo ilichezeshwa chini ya usimamizi wa bodi ya
michezo ya kubahatisha (Gaming Board) na kuwapata washindi hawa wanne
ambao leo tunakwenda kuwakabidhi zawadi zao”
Aidha
tarimo aliongeza kuwa Droo ya pili ya bahati na sibu hiyo inatarajiwa
kuchezeshwa mwezi wa Novemba mwaka huu na ya tatu itakuwa mwezi
Disemba ili kupisha zoezi la uuzaji wa Hisa litakaloanza tarehe
18/9/2017 na kutarajiwa kumalizika mwezi October
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...