Marehemu Mama Philberta Mapunda, mke wa aliyekuwa
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers – TSN),
Mzee Joseph Mapunda, amezikwa leo jioni Septemba 14, 2017 katika makaburi ya
Luguluni, Kwembe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam,
Marehemu Mama Mapunda, aliyefariki dunia
usiku wa Septemba 11, 2017 jijini Dar es salaam, alikuwa anasumbuliwa na
maradhi ya moyo na shinikizo la damu. Alikuwa na umri wa miaka 62.
Mume wa Marehemu, Mzee Mapunda, pia ni
mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Uongozi wa Michuzi Media Group na
wafanyakazi wote wanatoa pole kwa familia ya Mzee Mapunda na kuwatakia
uvumilivu katika wakati huu mgumu.
Mola na aiweke roho ya marehemu mahala pema
Peponi – Amina.
![]() |
Marehemu Mama Philberta Mapunda, mke wa aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers – TSN), Mzee Joseph Mapunda, ukiwasili nyumbani kabla ya kwenda mazishini |
![]() |
Ibada ya mazishi ya Marehemu Mama Philberta Mapunda |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...