Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) ametembelea shule ya msingi aliyosoma Tinde iliyopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga kisha kutoa msaada kwa wanafunzi nane wenye ulemavu wa viungo akiwemo kijana ambaye hawezi kuongea wala kutembea. Mbunge huyo ametembelea shule hiyo jana Jumatano Septemba 27,2017. 

Mheshimiwa Hilal ametoa msaada wa baiskeli kwa kijana ambaye hawezi kutembea wala kuongea anayesoma katika shule hiyo huku akijitolea kuwanunulia wanafunzi hao nane mahitaji yao yote ya shule mpaka watakapomaliza masomo yao ya shule ya msingi. 

“Hii shule nimesoma,baada ya kufika hapa nimeambiwa kuna watoto wenye ulemavu,baada kumuona kijana huyu nimempatia baiskeli lakini pia nimejitolea kuwahudumia wanafunzi hawa wanane ambao wana ulemavu wa viungo,nitawanunulia mahitaji yao ya shule na watakuwa wanakunywa uji kila siku kwa gharama zangu”,ameeleza Mbunge huyo. 

Mbali na kutoa msaada huo Mheshimiwa Azza Hilal ameshiriki zoezi la Upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga lililoanzishwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro lenye kauli mbiu ya "Shinyanga Mpya, Mti Kwanza". 

Akiwa katika kata ya Tinde,mbunge huyo aliungana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kupanda miti katika shule ya msingi Tinde,pia katika barabara kuu ya kutoka Tinde kwenda Kahama na barabara ya kutoka Tinde kwenda Nzega mkoani Tabora.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika shule ya msingi Tinde-Picha na Said Nassor-Malunde1 blog Tinde
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi Tinde,aliyeshikilia kipaza sauti ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...