Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. Aliwataka wajumbe hao kujadili namna ya kuwawezesha wakulima wa miti wakati wanasubiri kuvuna mazao yao waweze kujishuulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi kwa kutumia mbinu bora za kisayansi ili waweze kujikimu kimapato.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe
akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika
yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani
Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21
duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji
wa masoko.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi 21 duniani wakifuatilia mkutano huo. Nchi hizo ni Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Gambia,Ghana, Italy, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sudan, Liberia, Cameroon, Swaziland, Finland, Zambia, Canada,Mozambique, Zimbabwe, Kenya na Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe akizungumza katika mkutano huo. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kuishauri dunia namna bora ya kutunza na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwemo utekelezaji wa sheria za usimamizi wa misitu.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe kujadili kwa uwazi kuhusu mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za sekta ya misitu na kwamba Serikali kupitia Wizara itapokea maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuimarisha ustawi wa sekta hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...