Na Mwamvua Mwinyi ,Rufiji

Wakazi wa wilaya ya Rufiji ,Mkoani Pwani pamoja na watanzania kijumla wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (stiegler’s gorge hydropower dam project),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 .

Mradi huo utazalishwa kutoka chanzo hicho , katika pori la akiba la Selou Kanda ya Kaskazini (Matambwe ).Kwasasa nchi inazalisha megawatts 1,450 lakini Stiegler’s gorge itazalisha megawatts 2,100 hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi .

Akizungumza mara baada ya kwenda kukagua na kujiridhisha eneo utakapozalishwa mradi huo kabla ya utekelezaji kuanza,Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, alisema tangazo rasmi limeshatolewa na wizara ya nishati na madini tangu august 30 mwaka huu.

Aidha alifafanua ,tangazo hilo linawapa nafasi kwa makampuni ya ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme .Mhandisi Ndikilo,alibainisha kampuni yoyote iwe ya ndani ama nje ya nchi ikikidhidhi vigezo itatangazwa .
Alieleza endapo mradi utakamilika utawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na kuvutia wawekezaji kwa wingi.Mhandisi Ndikilo ,alisema wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kibiti na Rufiji umeme ukatikakatika hivyo kuna changamoto ya upungufu wa umeme hali inayokwamisha jitihada za kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akionyesha eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.(Picha na Mwamvua Mwinyi )
Eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme,linavyoonekana .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho karibu na pori la akiba la Selou .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,na ujumbe wake wakikagua eneo la mto huo.(Picha na Mwamvua Mwinyi ).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...