Jalada la kitabu
cha ‘MIFUPA YA ALBINO’.
Mwandishi Daniel Mbega, akiwa ameshikilia Karunguyeye waliokaushwa nyumbani
kwa mganga wa jadi.
MWANDISHI wa habari mwandamizi nchini, Daniel Mbega, amekamilisha
kuandika kitabu kinachofichua siri zilizo nyuma ya pazia kuhusiana na mauaji ya
vikongwe na albino nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Mwandishi huyo, ambaye alifanya utafiti kwa kipindi cha miezi nane
mfululizo katika mikoa 10 ya Kanda ya Maziwa Makuu, amesema kitabu hiyo alichokipa
jina la ‘MIFUPA YA ALBINO’ kinatarajiwa kuwaingia kiwandani wakati wowote na
kwa sasa anatafuta msaada wa fedha za kuchapia.
“Nimekamilisha, lakini nimekwama kidogo kuhusu fedha za uchapaji na
kama kuna taasisi yoyote au mtu anayeweza kunisaidia nitashukuru sana,” amesema
mwanahabari huyo.“Yeyote mwenye nia njema na jamii ya Watanzania na anaguswa
kusaidia uchapaji wa kitabu hiki, ninaomba awasiliane nami kwa namba hii 0656-331974, kwani naamini kitabu hiki
kitakuwa msaada pia wa kiroho baada ya kujua mambo yanayofanywa hata na baadhi
ya viongozi wa dini wanaotumia ushirikina,” aliongeza.
Bw. Mbega amesema kwamba, katika utafiti wake huo alifanikiwa
kukutana na waganga wa jadi, wachawi na matapeli katika mikoa ya Shinyanga,
Geita, Simiyu, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa, ambako
alikaa kwa miezi miwili akifanya uchunguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...