Baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul (Diamond Platinumz) kumwimba Mzee Onyango kuwa zilipendwa sasa mzee huyo ameibuka na kukana kuwa yeye sio Zilipendwa.
Hatimaye Mzee Onyango ambaye ni mwigizaji mkongwe nchini Tanzania amemjibu Diamond Platinumz kwa vitendo baada ya kuachia filamu yake mpya ya iitwayo BABU
THE PERFECT MAN kupitia kampuni yake ya ONYANGO PRODUCTION.
"Nashangaa sana kusikia Diamond Platinumz kuimba kwamba mimi na Mzee Jangala zilipendwa, mtoto huyu amenikosea sana mimi bado napendwa na mashabiki zangu bado wanaamini kuwa nina uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi ya uigizaji bila tatizo lolote" alisema Mzee Onyango.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...