Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa Simba umesema kuwa hauna mpango wa kuachana na kocha mkuu wa timu yao Mcameroon Joseph Omog kama kwenye vyoimbo vya habari na mitandao ya kijamii  walivyoandika kuwa wana mpango wa kumtema.

Akizungumzia suala hilo, Afisa habari wa Simba Hajji Manara, amesema Kamati ya utendaji ya klabu hiyo sambamba na Kaimu Rais Salim Abdallah wamezungumza na kocha Omog na kumueleza kuwa afanye anachoona kinawezekana katika kusaidia timu kufanya vizuri.

Manara amesema uongozi na kamati tendaji unamuamini kocha huyo huku wakiwataka mashabiki kumuacha kocha afanye kazi yake na kuacha kutunga maneno ambayo si kauli za viongozi wa klabu hiyo.

"Kumekuwa na tabia ya mashabiki kufurahia timu ikishinda na kuona ni timu yao lakini timu inapofanya vibaya wanamsukumia kocha na kuzusha kwenye mitandao mbalimbali kwa kusingizia uongozi umesema ili watugombanishe na benchi la ufundi", alisema Manara.

Mbali na hilo Manara amedai kuwa kwa sasa hawapo tayari kumfukuza kocha kwa kuwa wamejifunza kubadilisha makocha kila mara sio sababu ya kupata ushindi bali ni kujiweka pabaya zaidi.

Kuhusu mechi ya Simba na Mbao timu inaondoka kesho alfajiri huku akidai kuwa watakosa huduma ya wachezaji wao wawili akiwepo Said Mohamed 'Ndunda' ambaye anaenda India kwa matibabu na Shomari Kapombe ambaye ataanza mazoezi wiki hii.
Afisa habari wa Simba Haji Manara akizungumzia maamuzi ya kamati ya utendaji ya kutokuachana na kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon Joseph Omog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...