MAMLAKA ya  Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wametiliana saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano.

Mkataba huo uliosainiwa leo Dar es Salaam, utawezesha PPRA na NEEC kushirikiana   kiutendaji  ili kuwawezesha  wajasiriamali wadogo  na wa kati   kushiriki   kwenye fursa   mbalimbali  zinazopatikana katika manunuzi ya umma.

Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini  mkataba huo,  Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima, lengo linguine ni mamlaka  kuhakikisha  kigezo mojawapo  wakati wa  hatua ya tathimini kwenye zabuni za umma  cha  upendeleo kwa ajasiriamali  wadogo na kati kinazigatiwa.

“Pia  kila mwaka PPRA na NEEC kufanya tathimini ya pamoja ili  kujua namna taasisi nunuzi  zinavyotekeleza au kuzingatia ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wakati,”alisema Dk. Shirima.

Malengo mengine ni PPRA na NEEC kufanya tafiti za pamoja  zitakazo jikita  zaidi  katika uwezeshaji  na ushiriki wa wajasiriamali  wadogo na kati  kwenye michakato ya  manunuzi  ya umma.

“Suala la kuwajengea wananchi uwezo  wa kupambana na umasikini kwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi limekuwa  kipaumbele kikubwa  cha serikali na hasa ya awamu ya tano.

Ili kufanikisha azma hiyo , serikali imekuwa ikiandaa sera  na sheria  mbalimbali  zinazoweka mazingira  mazuri  ya wananchi  kushiriki na kuitumia fursa za kibiashara,”lifafanua Dk. Shirima.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima,akizugumza wakati  wa hafla ya utilianaji saini wa mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)  leo jijini Dar es Salaam.(kushoto)ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I  Issa.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima(kulia)pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano wanaoshuhudia  (kulia) ni  Mwanasheria Mwandamizi wa PPRA, Agnes Sayi  na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima, pamoja na wakibadilisha hati za mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...