Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Prof. Palamagamba John Kabudi, ametembelea ubalozi wa Tanzania Brusels, Ubeligiji tarehe 29 Septemba, 2017. Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji Mheshimiwa Joseph Edward Sokoine.
Prof. Kabudi yuko Mjini Brussels, Ubeligiji akiambatana na Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi.
Wakati akiwa Brussels, Prof. Kabudi ameshiriki mazungumzo baina ya Rais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi baina ya Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Prof. Palamagamba Kabudi,Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja Bw. Geoffrey Kabakaki, Mwambata Maalum (Minister Plenipotentiary) wakati alipotembea makazi ya Balozi.
Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji
Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...