Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka wenyeviti wa vijiji au wa mitaa kutojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababishwa na viongozi hao.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Masenza alisema kuwa kumekuwa na migogoro ambayo inasababishwa na wenyeviti wa serkali za vijiji au mtaa hivyo ni marufuku viongozi hao kujihusisha na swala hilo.

“Sipendi kusikia mwenyekiti wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji akihusisha kuwa shahidi wa uuzwaji wa ardhi kwa kuwa hilo sio jukumu lao waichie mamlaka ya ardhi kufanya kazi kwa utaalamu wao”alisema Masenza

Aidha Masenza alimtaka wakurugenzi wote wa mkoa wa iringa kuwaambia ukweli viongozi juu ya sheria ya uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro inayosababisha maumivu kwa upande unaonewa na kudhurumiwa haki yao ya msingi na kusababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo.

“Wakurugenzi waambieni vijana wetu waache ujanja ujanja wa kupokea,kuchora,kuonyesha na kuelekeza swala lolote linalohusu uuzwaji wa ardhi ili hii mipango kabambe ya halmashuri ziende vizuri kama serikali inavyopanga”alisema Masenza

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya ya mufindi wakati wa kutambulisha mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga uliokuwa na lengo la kuonyesha dira ya miaka ya hamsini (50) ya maendeleo ya mji wa Mafinga ambapo inasemeka ni moja kati ya miji inayokuwa kwa kasi .

hawa ni baadhi ya wadau waliojitokeza katika ukumbu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya mufindi kushuhudia utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...