NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), imeahidi kusimamia miradi ya umeme Kituo cha Tipper-Kigamboni,  Mbagala na Kurasini ili kuhakikisha inakamilika kwa haraka na kwa wakati na hatimaye wananchi wa maeneo hayo wanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, mwishoni mwa ziara yake ya kufuatilia uboreshaji wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha kufua na kusambaza umeme huko Kimbiji  wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam Septemba 18, 2017.

Waziri pia amekagua ujenzi wa mradi wa maendeleo ya upanuzi na upatikanaji nishati (TEDAP), wa kusafirisha umeme wa 132kv ulioko Gongolamboto nje kidogo ya jiji.

“Wananchi wanataka umeme, hawahitaji kujua  nguzo za umeme zimepatikana wapi, au upembuzi yakinifu utakamilika lini, nimeagiza baada ya siku tano kuanzia leo (Septemba 18), fanyeni kazi usiku na mchana walau vituo viwili vya kupoza na kusambaza umeme viwe vimekamilika ili wananchi wa Mbagala na Kigamboni wapate umeme wa kutosha.” Alisema Dkt. 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wakwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Khalid James, (watatu kushoto), wakimsikiliza Meneja Mradi wa TEDAP, Mhandisi Emmanuel Manirabona, (aliyenyoosha mkono), wakati Naibu Waziri na uongpozi wa TANESCO, ulipotembelea mradi wa TEDAP wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Septemba 18, 2017. Mradi huo unahusu upanuzi na uendelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme wa 132kv.


Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ambaye alifuatana naye kwenye ziara hiyo.
Sakafu ya kufungia transfoma mpya ya umeme wa 15mva kituo cha Tipper-Kigamboni, ikijengwa Septemba 18, 2017
Mshine mpya kwenye kituo cha Mbagala

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...