MCHEZAJI na Mwalimu wa Mchezo wa mpira wa Mgongo (Hoki), Osman Bairu aiomba Serikali kusaidia kujenga viwanja vya mpira wa Magongo hapa nchini.
Hayo amesema wakati akizungumza wa Michuzi Tv katika viwanja vya Tanganyika Pekazi jijini Dar es Salaam wakati wa mashindan ya mchezo wa Magongo uliohusisha Timu A na Timu B za shule ya Msingi Kawe jijini Dar es Salaam.Pia amewaomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kwenda kufanya mazoezi pamoja na ili mchezo huo upate kwenda mbali zaidi.
Mwalimu na Mchezaji wa mpira wa Magongo (Hoki), Osman Bairuakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu A na Timu B kabla ya mashidano yati ya Timu Hizo mbili za kutoka Shule ya msing Kawe B jijini Dar es Salaam.
Mwalimu na Mchezaji wa mpira wa Magongo (Hoki), Osman Bairu akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es Salaam wakati wa mchuano wa mchezo wa Magongo kati ya Timu A na Timu B ya shule ya Msingi Kawe B jijini Dar es Salaam .Ambapo Mchezo huo ulifana sana na Timu ya ya mchezo huo waliweza kufungana 5-2 Timu A walifunga mabao matano na Timu B walifuga mawili.
Wachezaji wa Timu A wakijaribu kunyang'anya Mpira Mchezaji wa Timu B wakati wa Mashindano ya Kirafiki uliofanyika katika viwanja vya Tanganyika Pekazi jijini Dar es Salaam.
Mchezo ukiendelea kati ya Tmu A na Timu B za shule ya Msingi Kawe B jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...