Na Mathias Canal, Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Septemba 7, 2017 Amezindua Programu maalumu kwa Vijana wa CCM katika ushiriki wa shughuli za miradi ya Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii katika ukumbi wa CCM (NEC) Mjini Dodoma.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Shaka alisema Wazo hilo limeibuliwa wakati muafaka huku serikali ya CCM awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ikiweka mkazo na vipaumbele kadhaa vinavyomtaka kila mtanzania hususani vijana kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha Mali.

Alisema dhana ya
kufanya kazi kwa bidii, malengo na shabaha si ngeni lakini kwa wakati
huu inahubiriwa kwa nguvu kulingana na changamoto nyingi zilizopo,
fursa, ushirikishwaji kwa kuzingatia mahitaji halisi kutokana na
mabadiliko ya dunia Kiuchumi na Kimaendeleo.
Aliwasisitiza Vijana kutambua wajibu wa kukuza shughuli za kazi na maisha zikiongozwa na nguvu ya uzalendo, kujali utaifa na kutambua dhamana iliyopo ya kudumisha amani, Umoja, Mshikamano na Maendeleo."Ili kusihi yote hayo hatimaye Vijana waweze kuyafanikisha tunapaswa kuwa na mioyo isiyopwaya au kukosa rutuba ya kutodumisha uzalendo, tunalazimika kwa pamoja kutambua mpango wowote wa kuyafikia maendeleo ya kweli utabaki ni hadithi na ndoto Kama hatutaongozwa na shime ya uzalendo au kutothamini utaifa wetu Kama ambavyo viongozi wanatuhimiza siku Hadi siku" Alisema Shaka.

Shaka aliwaeleza Vijana kuwa pamoja na kuwepo juhudi kubwa za mara kwa mara kuchukuliwa na serikali, mashirika hiari ya Kijamii na yasiyokuwa ya kiserikali, kuelimisha juu ya dhana ya ushirikishwaji na ushiriki wa Vijana katika miradi ya Kiuchumi na Kijamii wanapaswa kuwa na utayari, uthubutu, uzalendo, na Utaifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...