Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wazee wote wa mkoa wa Dar-es-salaam Wilaya ya Ubungo kuwa zoezi la Usajili na Utambuzi lenye lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa
linaendelea sambamba na zoezi la Usajili wa Kadi za Bima ya Afya kwa wazee
chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Wahusika ni wazee
wote wanaoishi Wilaya ya Ubungo. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua na kujaza fomu
ya maombi ya Usajili. Fomu zinapatikana ofisi
ya Mtaa unakoishi au Ofisi ya Kata. Unapojaza fomu ya maombi unatakiwa kuweka
na nakala ya viambatisho muhimu vinavyokutambulisha
vile ulivyonavyo mathalani Kadi ya Kupigia kura, Barua ya Serikali ya Mtaa,
vyeti vya shule na kisha fika na fomu yako ikiwa imejazwa pamoja na vivuli
(photocopy) ya viambatisho hivyo kwenye kituo cha karibu kusajiliwa.
Unapofika kusajiliwa
unashauriwa kwa ajili ya ubora wa picha kutovaa nguo nyeupe, kijivu, bluu,
pinki, au rangi yoyote inayoshabihiana na nyeupe, nguo zenye nembo, kofia aina
yeyote ama kupaka hina kwenye viganja vya mikononi.
Kwa kuanza wiki ijayo Ratiba ya Usajili itakuwa ni kama ifuatavyo:-
Na
|
KITUO CHA USAJILI
|
MUDA
|
TAREHE
|
1.
|
Kata ya Makurumla
|
Saa 3:00 – 11:00
jioni
|
11/09/2017
|
2.
|
Kata ya Manzese
|
Saa 3:00 – 11:00
jioni
|
12/09/2017
|
3.
|
Kata ya Sinza
|
Saa 3:00 – 11:00
jioni
|
13/09/2017
|
4.
|
Kata ya Makuburi
|
Saa 3:00 – 11:00
jioni
|
14/09/2017
|
Utaratibu wa Usajili katika Kata zingine tutaendelea
kuwafahamisha. Kupata maelezo
zaidi tafadhali wasiliana na mtendaji wako wa Mtaa au Mtendaji Kata.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Vitambulisho vya Taifa tembelea
Tovuti yetu www.nida.go.tz au ukurasa wetu wa facebook -nidatanzania au twitter
@nidatanzania
Wazee jitokezeni kusajiliwa Vitambulisho
vya Taifa ili mtambulike na kupata huduma za kijamii kwa haraka na kwa uhakika zaidi.
Limetolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...