Ajali mbaya iliyohusisha magari mawili, Lori na Basi ndogo aina ya Toyota Coaster, imetokea karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka huko Kampala, Uganda, usiku wa kuamkia leo Septemba 18, 2017.
Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.
Basi hilo dogo lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikuja kwenye harusi tarehe 16/09/2017 hapa Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es salaam.
Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.
Naibu Balozi Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona Walio nusurika.
Lori na Basi ndogo aina ya Toyota Coaster yaliyohusika kwenye ajali hiyo.
Lori na Basi ndogo aina ya Toyota Coaster yaliyohusika kwenye ajali hiyo.
Majina yaliyopatikana kufuatia ajali hiyo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI -AMEN
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...