
Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) limesema linaunga mkono juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya Taifa jambo ambalo litasaidia kuchangia kwa kasi harakati za kimaendeleo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini ambapo alisema tokea Serikali ya awamu ya tano iingie madaraka inakaribia kutimiza miaka miwili lakini ndani ya kipindi hicho watanzania wameona mambo mengi makubwa yakifanywa kwa ajili ya kuipa nchi maendeleo.
Alisema moja kati ya mambo makubwa ni suala la kiongozi huyo kupamaba na vita dhidi ya dawa za kulevya,kuondoa watumishi hewa serikalini pamoja na wenye vyeti feki, Vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi,kufufua shirika letu la Ndege(ATC) kwa kununua ndege ambazo hivi sasa watanzania wanajivunia kuwa ni mali yao.
Mwenyekiti huyo alisema pia mambo mengine ni Ujenzi wa Reli ya kisasa, Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), utoaji wa ajira zaidi ya 50,000 kwa vijana wahitimu, Kuimarisha utumishi wenye nidhamu na uwajibikaji serikalini, Kuinua kwa kasi uchumi wa nchi yetu kimataifa, Kuboresha sekta ya afya pamoja na kupunguza bei za madawa ya binadamu nchini na mengine mengi yaliyoleta maendeleo ya nchi yetu
Alisema pamoja na hayo lakini Rais Magufuli alionyesha ujasiri mkubwa kwa kuzuia mchanga wa madini ya dhahabu (Makinikia) na kuunda tume ili ichunguze namna nchi ilivyokuwa inapoteza mapatoambayo ilionyesha jinsi watu walivyoibiwa mapato ya Taifa kwa kipindi kirefu.
“Lakini hakuishia hapo Juzi Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Madini ya Almas na Tanzanite iliyochunguzwa na kamati mbili zilizoundwa na Mhe. Spika Jobu Ndugai ripoti ambayo imeonyesha jinsi watanzania tulivyoibiwa kwa kipindi kirefu, Mhe. Rais hakusita kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kupelekea Taifa kupoteza mapato”Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...