Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeungana
na kampni inayotoa huduma za usafiri Twende App kuzindua huduma mpya
itakayowezehsa wasafiri kupata huduma bora, ya haraka na uhakika zaidi
kupitia mfumo wa simu za mkononi unaojulikana kama Twende App.
TwendeApp
ni mfumo wa kidigitali wa simu za mkononi unaowezesha wasafiri kutafuta
na kupata usafiri wa taxi, pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda) na
zile za magurudumu matatu kupitia simu zao za mkononi kwa uhakika
zaidi na kwa bei nafuu.
Twende
App ambayo, tayari inatumika katika jiji la Dar es salaam, sasa
imepanua wigo wake na kufikia miji ya Arusha, Morogoro, Mwanza,
Kilimanjaro, Dodoma Iringa na Mbeya. Kuna mipango ya kusambaza huduma
hiyo kwenda Zanzibar, Tanga na Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...