Na Khadija Khamis –Maelezo

Jamii inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na meno ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya angalau mara mbili kwa mwaka .

Hayo aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .

Alisema afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza meno .Alifahamisha kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .

Aidha alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na vijijini .

“Huu usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...