Chama Cha Mapinduzi, kimefafanua kuhusu Katibu Mkuu wa Chama hicho, ABDULRAHMAN KINANA, kutohudhuria Kikao cha Kamati Kuu, kikisema kwamba hakuhudhuria Kikao hicho kutokana na kupata Dharura ya Kihali ya Ki-Utu. 

Hata hivyo, kimesema kazi yote ya Maandalizi ya Kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC, kinachoanza kesho imefanywa na KINANA. 

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, HUMPHREY POLEPOLE, amesema Kamati Kuu katika kikao chake ilipata taarifa rasmi kupitia kwa Mwenyekiti Rais JOHN MAGUFULI kwamba Katibu Mkuu ameomba udhuru wa kihali. 

Katika hatua nyingine, Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC, wameanza kuwasili jijini Dar es salaam, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba kwa ajili ya kukamilisha taratibu muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao hivyo muhimu vya Chama.

Kuanza kwa kikao hicho kesho kunatokana na kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ambacho kilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Rais JOHN MAGUFULI. 

Pamoja na mambo mengine, POLEPOLE, amesema vikao hivyo vya maamuzi vina kazi ya kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wana-CCM-wanaoomba ridhaa ya nafasi ya Uenyekiti wa CCM ngazi ya Wilaya. 

Kikao cha NEC kitafanyika kwa siku Mbili, Jumamosi na Jumapili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...