Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akipokea msaada wa vifaa
mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Anayekabidhi vifaa hivyo
ni, Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi. Vifaa hivyo vina
jumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na kuchapishia vyenye thamani ya Dola
za Kimarekani elfu arobaini. Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na wana habari
nimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es
Salaam.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala kwa pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini Tanzania, Dkt. Qassim Sufi wakisaini nyaraka za makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika hilo, katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam leo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akibadilishana nyaraka za
makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la
Uhamiaji (IOM) na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania, Dkt. Qassim Sufi, katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam leo. Vifaa hivyo vina jumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na
kuchapishia vyenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu arobaini.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...