Na mwandishi wetu, Kondoa.
Uingizaji wa mifugo kwenye pori la akiba la Mkungunero lililoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma umeathiri uhifadhi wa pori hilo na kusababisha kukauka kwa baadhi ya vyanzo vya maji na kutoweka kwa baadhi ya wanyamapori adimu.
Meneja wa Pori la akiba la Mkungunero, Emmanuel Bilaso akizungumza na a waandishi wa habari waliotembelea pori hilo hivi karibuni amesema pori hilo linalopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire lina vyanzo muhimu vya maji ambayo yanayotegemewa na wananchi wengi kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Bilaso amesema pori hilo la Mkungunero pia lina vyanzo vya maji ya mto Tarangire ambao ndiyo uhai wa Hifadhi ya taifa ya Tarangire na akatoa wito kwa wananchi kutilia mkazo uhifadhi ambao una umuhimu mkubwa kwa jamii na maendeleo ya taifa.
Amesema operesheni inayoendelea katika pori hilo imefanikisha kukamata kwa mifugo mingi katika pori hilo ambayo inachunga humo kinyume na sheria ya uhifadhi ambayo inakataza shughuli za binadamu kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
“Tumekamata ng’ombe zaidi ya 230 ambao waliingizwa na wananchi kinyume cha sheria na wamefikishwa mahakamani na kutozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 6” alisema bwana Bilaso.
Aliongeza kuwa kuingiza ng’ombe ndani ya hifadhi ni kinyume cha sheria ya uhifadhi ambayo inatoa adhabu kali ikiwemo kutaifisha mifugo inayokamatwa ili iwe fundisho kwa watu wanaovunja sheria za uhifadhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...